
Meya Mwita ameyasema hayo katika kipindi cha HOTMIX kinachorushwa na EATV kila siku ya jumatatu hadi ijumaa wakati akijibu swali kuhusu ushirikiano wake na viongozi wengine wa serikali katika kuleta maendeleo ya wananchi.
''Mimi nina muda wa mwezi mmoja ofisini sina tatizo na Mkuu wa Mkoa kwa sababu uchaguzi umeshakwisha wananchi wanachokitaka ni maendeleo hivyo tunashirikiana vyema''- Amesema Meya.
Aidha Meya amesema kwamba stendi ya Ubungo ilibomolewa na uongozi uliopita kimakosa kwani malengo ambayo yaliwekwa kwa kubomoa stendi hiyo hayakutekelezwa.