Rais huyo pia amesema kwamba tangu jana (Februari 22, 2016) nchi hiyo imepokea ugeni mkubwa wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Ban Ki-moon na inatarajia kupokea marais watano kutoka nchi za Umoja wa Afrika tarehe 25 Februari, 2016.
Ujumbe wa Rais Nkurunziza umewasilishwa na Mjumbe maalum ambaye pia ni Waziri wa Afrika Mashariki wa Burundi, Mheshimiwa Leontina Nzeyimana leo tarehe 23 Februari, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, alipokutana na Rais Magufuli na kufanya nae Mazungumzo.
Pamoja na kumpa taarifa kuwa Burundi inaendelea vizuri, Mheshimiwa Nzeyimana pia amemueleza Rais Magufuli kuwa Burundi ipo tayari kupokea nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka kwa Rwanda, ikiwa ni kwa mujibu wa Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaoelekeza kuwa nchi inayofuata kutoa Katibu Mkuu baada ya Katibu Mkuu wa sasa kumaliza muda wake, ni Burundi.