
Waziri mkuu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na kamati ya amani ya mkoa wa Dar es salaam kwa kutambua mchango wao katika kuimarisha amani katika jiji la Dar es salaam na nchini kwa ujumla.
Majaliwa amesema alishangazwa kuona kupitia runinga mtanzania aliyekuwa anawasafirisha wasichana wawili kwenda nje ya nchi kufanya kazi za majumbani.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye ulemavu) Dkt Abdallah Possi amewataka viongozi wa dini nchini kutumia busara hasa wanapozungumza masuala ya kisiasa ili kudumisha amani hapa nchini.
Aidha kamati ya amani mkoa wa Dar es salaam wameahidi kuendeleza mshikamano wao kwa lengo la kuendelea kulifanya jiji la Dar es salaam kuwa na amani na utulivu.