Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema kuwa mtu huyo alikamatwa baada ya Bw. Kelvin Nyerere kutoa taarifa ya kutapeliwa pale alipotaka kununua madini ya dhahabu ya Kg 20 na kuuziwa vipande vitau vya madini bandia.
Amesema jeshi la polisi limebaini vielelezo vingine nyumbani kwa mtuhumiwa ikiwa ni pamoja na madini ya bandia, chuma cha kuchomea madini, mashine ya kupimia madini, vifaa vya kubainia madini, mashine ya kupimia madini, hati za usajili wa kampuni ya Crown Logistic and Cargo Handling Limited na risiti mbalimbali zinazoonesha kuwa madini yameuzwa kwa wateja wengine.
Jeshi la polisi linatoa tahadhari kwa wale wote wanaonunua madini kujiridhisha na uhalali wa madini hayo kabla hawajayanunua kwani kunaonekana kuna mtandao mkubwa wa matapeli hao.