Mkuu wa mkoa amefanya maamuzi hayo wakati akihutubia katika sherehe hizo zilizofanyika kimkoa katika halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu ambapo amewataja wanaotuhumiwa kuwa ni Shaibu Mwakakita, Haswege Kaminyonge na Kheri Kagogoro wa halmashauri ya mji wa Masasi pamoja na Suleiman Katete wa halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu.
Kuhusu wafanyakazi hewa, amesema mpaka siku moja kabla ya maadhimisho hayo mkoa wa Mtwara ulikuwa na wafanyakazi hewa 107 huku zaidi ya sh. Milioni 300.9 zimepotea, ambazo zingesaidia kulipa madeni ya uhamisho na masaa ya ziada kwa wafanyakazi.
Akizungumza kwa niaba ya katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) mkoa wa Mtwara, Ado Chiwangu, Katibu wa Chama cha Walimu Mkoa wa Mtwara (CWT), Fratern Kwahisson, amesema kaulimbiu ya mwaka huu inayosema “Nidhamu ya mabadiliko iinue hali ya wafanyakazi”, inalenga kuitaka serikali, waajiri na wadau wengine wa ajira kuboresha ustawi wa wafanyakazi ili kuleta tija.