Naibu Waziri Wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani (Kushoto).
katika kutangaza maliasili za Taifa pamoja na nchi yenyewe kwa kuwa ni ya kipekee.
Mhandisi Ramo ameeleza hayo wakati akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio huku akiwataka watanzania kutumia simu zao za mikononi kutuma ujumbe au picha zinazoelezea utalii wa ndani hasa Mlima Kilimanjaro.
"Moja ya jambo tulilojiwekea ni kuongeza jitihada katika kutangaza vituo vya utalii tulivyo navyo na kuitangaza Tanzania kama nchi yenye vivutio vya pekee na huo upekee wake duniani ndiyo unawavuta sasa watu wajiulize kuna nchi hii iliyopo katika bara la Afrika". amesema Mhandisi Makani.
Mhandisi Makani ameendelea kwa kusema "tunaitangaza Tanzania kama 'unique tourism of the nation', ukishamwambia mtu Tanzania ni tofauti na vituo vyake vilivyopo ni vya tofauti lazima atavutiwa aje kuviona", amesisitiza Mhandisi Makani.
Miongoni mwa watu maarufu waliotembelea vivutio hivyo, hivi karibuni ni pamoja na msanii maarufu wa filamu za Bolywood nchini India Sanjay Dutt, Will Smith na familia yake, mchezaji wa zamani wa timu ya Liverpool Mamadou Sakho, mcheza soka maarufu David Beckham, mwanamuziki wa Marekani Usher Raymond, Victor Wanyama, Leon Osman, Christian Ericksen pamoja na muigizaji na mtayarishaji filamu maarufu duniani Harrison Ford.
Kwa upande mwingine, mtandao wa kimataifa wa kibiashara 'SafariBookings.com' umeitangaza Tanzania kuwa nchi ya kwanza Afrika inayowavutia zaidi watalii baada ya kuchukua maoni ya watalii zaidi ya 2,500 waliotembelea nchi za Afrika na idadi kubwa waliitaja Tanzania kuwa bora kuliko nchi nyingine.



