Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Sakata la utoro Bungeni, Lema amjibu Spika

Friday , 16th Nov , 2018

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekiri kuwa na mahudhurio hafifu ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kile alichokisema kuwa ni kukabiliwa na majukumu mengine ya nje ya ubunge, ambapo aliitaja sababu ya kuhudhuria kesi mbalimbali mahakamani.

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, Spika wa Bunge Job Ndugai/.

Kauli hiyo ya Lema imekuja siku moja baada ya Spika Job Ndugai kumtaja mbunge huyo pamoja na Mbunge wa Kibamba John Mnyika wako kwenye orodha ya wabunge ambao wana mahudhurio hafifu kwenye bunge la hilo.

Akizungumza na www.eatv.tv Lema amesema “sisi ni wabunge ambao tuna kesi nyingi mahakamani, kwenye bunge la bajeti nilihudhuria mahakamani mara 4 kwa mwezi, kwa misingi kama hiyo lazima utakuwa na mahudhurio hafifu bungeni.”

Mimi pia nimekaa jela miezi 5 na spika amesahau kule jela hakuna bunge, na nilikamatwa wakati wa bunge na nikaachiwa kipindi ambacho bunge limeisha,” ameongeza Lema

Kingine huwezi kuhudhuria bungeni kila siku, ni lazima uwe na hoja mimi mahudhurio yangu huwa yanamchango sana kwa taifa hasa kwenye uchumi, siasa na haki za binadamu lakini wao wanawabunge wengi ambao wanahudhuria bungeni kama wanafunzi wa darasa la kwanza,” ameongeza Lema.

Aidha Lema amesema “Lakini mimi ni mwakilishi wa jimbo kuna wakati naenda kufanya kazi jimboni au kuwatafutia misaada wananchi wangu, pia mbunge ni mwakilishi wa chama mimi kwangu nimefanya uchaguzi mara mbili kwa hiyo nisingeweza kuhudhuria bunge".

Yapo mengi sana lakini bado uwepo wetu kila tunapopata nafasi ya kuingia bungeni huwa tunatoa michango ambayo ni muhimu sana kwa taiifa,” amemalizia Lema.

HABARI ZAIDI

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Wanahabari wasisitizwa kuzingatia maadili ya kazi

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC atangaza msako kuwaondoa walinzi wazee kazini