
Naibu Waziri huyo ameyasema hayo wakati akikagua mradi wa maji wilayani Momba Mkoani Songwe.
"Serikali inataka mradi huu na miradi mingine yote ya maji nchini ikamilike kwa wakati na wananchi waanze kufaidi matunda ya Serikali yao, ndio maana nipohapa kufuatilia hilo na wakandarasi waliopewa kazi wahakikishe wanafanya kazi usiku na mchana ili kufanikisha hilo la si hivyo serikali haitasita kuwachukulia hatua.,’’ amesema Mh. Aweso.
Naibu Waziri huyo yupo Mkoani Songwe katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali