Wednesday , 21st Nov , 2018

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linawashikilia watu sita kwa makosa ya kuvunja nyumba usiku na kuiba vitu mbalimbali vikiwemo friji, tv, radio, majiko, computer, king’amuzi, pasi, laptop na spika za radio katika kata ya igogo wilayani Nyamagana huku wawili wakiuza vitu hivyo kwa watu

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna.

mbalimbali ilhali wakijua kuwa ni vitu vya wizi.

Ni katika oparesheni kabambe inayoendelea kufanywa na jeshi la polisi katika kata ya Igogo wilayani Nyamagana ya kuwabaini watu wanaofanya vitendo vya uvunjifu wa amani katika mitaa mbalimbali na kuweza kuwabaini watu hao sita.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna amewataja watu hao kuwa ni, willium Alex (24),  dereva wa bodaboda, Peter Deogratius (24), David Yussuph (18) dereva bodaboda na Godfrey Joseph (28) huku waliokuwa wanavipokea vitu hivyo vya wizi na kisha kuviuza ni Rashidy Ramadhani (32) na Esther Isack (55).

Baadhi ya wakazi walioibiwa vitu vyao wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa hatua hiyo, mara baada ya kuvitambua vitu hivyo.

Jeshi la polisi limetoa wito kwa wakazi hasa vijana wanaojihusiha na vitendo vya uhalifu kuacha mara moja kwani ni kosa la jinai na kwamba watakaobainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.