Tuesday , 2nd Jan , 2018

Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi (Sugu)  pamoja na Katibu wa Chadema, Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga, wameachiwa huru baada ya kuhojiwa kwa saa kadhaa katika Makao Makuu ya Polisi Mbeya.

Taarifa iliyotolewa leo na CHADEMA, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, imesema, kuhojiwa kwa viongozi hao kunatokana na wito wa polisi uliowataka waripoti siku leo ili kuhojiwa kuhusiana na maneno ya “uchochezi” wanayodaiwa kuyatoa katika mkutano wa hadhara wa mbunge huyo uliofanyika Disemba 30 mwaka jana.

Mh. Mbilinyi amewaambia waandishi wa habari kwamba, ni kweli waliitwa na polisi na kuhojiwa na kikubwa walichoeleza ni kuwa wao kama viongozi katika jamii wanapaswa kupongeza na kukosoa serikali pale inapobidi sababu ndio majukumu yao ya uwakilishi wa wananchi..

Viongozi hao wametakiwa kuripoti polisi tena Ijumaa Januari 5.