Monday , 12th Nov , 2018

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi amesema wadau wengi hawajitokezi kusaidia kwenye masuala ya elimu kwa sasa kutokana na sera ya elimu bure ambayo imepelekea serikali kufuta ada.

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi "Sugu".

Kwa mujibu wa Joseph Mbilinyi "Sugu" fedha anazopata kupitia muziki wake umekuwa ukisomesha zaidi ya wanafunzi 400 katika kituo cha watoto anachokilea na kuomba msaada kutoka kwa wadau wajitokeze kusaidia elimu.

Joseph Mbilinyi amesema " kwa miaka ya nyuma kabla ya ada bure nilikuwa tunawalipia ada, japo sitegemei zaidi kuhusu kipato cha mziki nina vyanzo vingine vya mapato."

"Bahati mbaya sasa hivi kutokana na sera ya elimu bure, mashirika na taasisi nyingi hawajitokezi kusaidia kwa wataonekana wanaenda kinyume na sera ya elimu, bure lakini kiuhalisia wamefuta ada tu ila bado kuna uhitaji mkubwa sana hasa kwa watoto wenye uhitaji maalum naomba wadau wajitokeze." Amesema Sugu

Sugu ni miongoni mwa wasanii ambao walifanikiwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akiwa sambamba na Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay  ambaye aliingia katika siasa na kufanikiwa kushinda ubunge kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.