Friday , 22nd Jan , 2016

Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania (TACAIDS) leo imezinduwa ripoti ya tathmini ya mazingir

Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania (TACAIDS) leo imezinduwa ripoti ya tathmini ya mazingira ya kisheria katika mwitikio wa UKIMWI, huku ikibanisha kubadilishwa baadhi ya sheria ili kuendana na wakati katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Akizungumzia ripoti hiyo iliofanywa kwenye mikoa 11 Mkurugenzi Mtendaji wa tume hiyo visiwani Zanzibar, Dkt. Ali S. Ali amesema ripoti hiyo imeainisha maeneo ya kisheria yanayotakiwa kubadilishwa ikiwa ni pamoja na kujumuishwa kwa makundi maalumu kama wanaouza miili yao, madereva malori, bodaboda pamoja na kuthibiti unyanyapaa na ubaguzi uliokithiri katika jamii kwa wagonjwa wa UKIMWI.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha Sheria wa (TACAIDS) Bi. Elizabeth Kaganda amesisitiza kubadilishwa kwa sheria za ndoa ya mtoto ili zioane na matakwa ya sheria ya UKIMWI ikiwa ni pamoja na kuruhusu watoto walio chini ya umri wa miaka 18 waruhusiwe kupima afya zao bila idhini kutoka kwa wazazi wao