Tuesday , 18th Jul , 2017

Tanzania inatumia zaidi ya shilingi bilioni 600 kila mwaka kwa ajili ya kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi fedha ambazo zingeweza kutumiwa kwa ajili ya shughuli nyingine za kimaendeleo iwapo mafuta hayo yangezalishwa hapa nchini.

Mkurugenzi wa Sera na Utafiti kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi nchini  (TPSF) Bw. Gili Teri.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Sera na Utafiti kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi nchini  (TPSF) Bw. Gili Teri wakati akitoa matokeo ya utafiti uliyofanywa na Taasisi hiyo kuhusu sekta ndogo ya mafuta na namna nchi inavyoweza kujitegemea kwa bidhaa hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo.

Aidha, Teri amefafanua kwa kusema utafiti huo unaonyesha kuwa ipo haja ya Tanzania kama nchi kuendelea na uagizaji wa mafuta kutoka nje ya nchi huku ikiendelea na uzalishaji wa ndani ambao hivi sasa umefikia tani za ujazo laki 1 na elfu 80 kati ya takribani tani laki tano zinazohitajika kwa kila mwaka.