Thursday , 2nd Apr , 2015

Serikali imesema jumla ya watanzania milioni 12.3 wanaakaunti za kutuma na kupokea pesa kwa kutumia mitandao mbalimbali ya simu nchini.

Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia Prof Makame Mbarawa.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa wakati akitoa hoja ya kuhitimisha miswada ya Sheria ya Makosa ya Mitandao na Muswada wa Miamala ya Kielektroniki.

Prof. Mbarawa amesema kwa kutumia mfumo huo zaidi ya shilingi trilioni 28.3 zimetumwa na wateja wa mitandao hiyo kupitia huduma za simu za mkono.

Ameongeza kuwa makampuni hayo ya simu pia yametoa ajira kwa watu laki mbili pamoja na ajira milioni 1.5 sizizo za moja kwa moja.