Tuesday , 3rd May , 2016

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Tanzania – TUCTA Bw. Nicholous Mgaya, amesema licha ya uchumi wa nchi kukua kwa kiwango cha asilimia 7 kwa mwaka, bado ukuaji huo hauendi sambamba na uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Tanzania – TUCTA Bw.Nicholous Mgaya

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Tanzania – TUCTA Bw. Nicholous Mgaya, amesema licha ya uchumi wa nchi kukua kwa kiwango cha asilimia 7 kwa mwaka, bado ukuaji huo hauendi sambamba na uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi ambao wamekuwa wakiishi maisha ya dhiki na ufukara.

Mgaya amesema hayo jijini Dar es Salaam leo katika mahojiano na EATV na kuongeza kuwa ofisi yake inashangaa kuona wafanyakazi nchini wakiendelea kuishi maisha ya ufukara tofauti na mtazamo wa baadhi ya watafiti wanaosema kuwa uchumi wa nchi umekuwa ukikua kwa kasi ya kuridhisha.

Katibu Mkuu huyo wa TUCTA ameiomba serikali iendelee kusimamia vizuri uchumi sambamba na kuongeza thamani ya shilingi ya Tanzania, huku ikihakikisha kuwa maendeleo ya nchi yanaenda sambamba na uboreshaji wa hali za wafanyakazi kwani wamekuwa wakikatwa kodi kubwa ambazo haziendani na huduma wanazopata.