Wednesday , 2nd Nov , 2016

Ukosefu wa mabweni katika shule za sekondari zilizopo maeneo ya vijijini imeelezwa kuwa kikwazo kinachochangia watoto wa kike kushindwa kuendelea na masomo hivyo kukwamisha jitihada za serika katika kuhakikisha kila mtoto anapata elimu.

Mbunge wa Hanang, Mhe. Dkt. Marry Nagu.

 

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Genda iliyopo katika wilaya ya Mbulu mkoa wa Manyara, katika harambee ya ujenzi wa bweni la wasichana wa shule hiyo, inayokabiliwa na uhaba mkubwa wa mabweni iliyoongozwa na Mhe. Marry Nagu ambaye pia ni mbunge wa Hanang.

Naye Mbunge huyo amesema njia pekee ya kuondokana na umaskini, jamii inapaswa kubadili mtazamo kwa kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu bora ili kuwa na jamii ya watu wenye uwezo wa kumudu mazingira yao na kuleta maendeleo.

Mkuu wa shule ya Genda Nicolaus Genda amesema kwa sasa shule yake inapokea watoto wengi wa kike hali inayoonesha kuwa jamii imeaanza kuhamasika katika kuwapa watoto wa kike elimu licha ya changamoto mbalimbali.

Kwa sasa zaidi ya wanafunzi 200 wa kike hawana bweni, ambapo katika harambee hiyo zaidi ya shilingi milioni 45 zimepatikana kutoka kwa wadau mbalimbali .