
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid.
Akiongea leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la AMREF Africa, Tanzania Dkt. Rita Noronha amesema kufuatia hali hiyo wameanza mpango wa kutoa elimu ya masafa kwa wakunga na wauguzi walio katika vituo vya afya vijijini ili waendelee kuboresha ujuzi wao.
Dkt. Noronha amesema kupoteza maisha kwa wanawake hao pamoja na watoto kunachangiwa na sababu nyingi ikiwa ni pamoja na uchache wa wakunga hivyo mpango huo wa masomo kwa njia ya masafa unaojulikana kama e-learning utawasaidia wauguzi kujiendeleza kielimu wakiwa katika vituo vyao vya kazi.
Wakati huo huo, washtakiwa sita wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kusomewa makosa manne likiwemo la kufanya ugaidi kwa kulipua bomu kwenye mgahawa wa Vama, uliopo eneo la uzunguni na kusababisha majeruhi wanane.
Wakisomewa hati ya mashitaka na Wakili wa serikali, Augustino Kombe mbele ya hakimu wa mahakama hiyo , Rose Ngoka, amesema washitakiwa walikula njama za kufanya ugaidi kwenye mgahawa wa Vama.
Hakimu wa Mahakama hiyo, Rose Ngoka, hakuruhusu washitakiwa hao kuongea chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo hadi hapo kesi itakapotajwa tena Agosti 6 mwaka huu.