Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Viongozi kukaa madarakani miaka saba!?

Thursday , 14th Sep , 2017

Mbunge wa jimbo la Chemba, Juma Nkamia (CCM) amethibitisha kuwa leo atapeleka hoja binafsi kwa spika wa bunge kuhusu uchaguzi mkuu nchini ufanyike kila baada ya miaka saba na isiwe mitano kama sasa ili kuepuka gharama kubwa ambazo huwa zinatumika.

Mbunge Juma Nkamia

Akifanya mahojiano kwa njia ya simu na mtangazaji wa EATV, Mh. Nkamia amesema kuwa yeye ameamua kupeleka muswada huo binafsi kwa spika wa bunge kutokana na serikali kutumia gharama kubwa za kufanya uchaguzi kwa wakati mmoja yaani ule wa serikali za mitaa pamoja na ule mkuu.

"Napeleka hoja au muswada binafsi kwa Spika wa bunge tulijadili hili kama linaweza kufanywa sheria lifanyike.  Ndani ya bunge kuna viongozi wetu wa chama kwa hiyo lazima nipeleke kwao ili kujadili na wao waweze kupitisha kama watakubaliana na mimi na kama ikifanikiwa kufika kwa rais basi iwe sheria ambayo itatuoongoza," amesema Nkamia.

"Nikipeleka hoja yangu kwa Spika nitachanganua gharama zinazotumika kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja uchaguzi mkuu. Tunaweza kufanya uchaguzi wote kwa pamoja kama wenzetu mfano Kenya wanakuwa na maboksi mengi sana wakati wa kura, hata sisi tunaweza kufanya kama wenzetu badala ya kutumia gharama mbili kwa kipindi kimoja" aliongeza Nkamia.

Aidha, Mh. Nkamia amefafanua kuwa aeleweke kuwa hajamlenga rais aliyoko madarakani ndiye aanze kwenda miaka saba bali ni kwa viongozi wote na kama wazo lake likitimia wakati Rais Magufuli akiwa madarakani nayo si vibaya.

"Muswada una 'process' zake kwani lazima upitie sehemu nyingi na kama ukishafika kwa wabunge ukajadiliwa na ikakubalika sheria ifanyiwe mabadiliko ndani ya sheria na rais akatia saini ndiyo itakuwa sheria kamili. Na ukifanikiwa kupita wakati Rais Magufuli akiwa madarakani ni vema tu kwani kuna matatizo gani?:", amehoji Nkamia.

Pamoja na hayo Mh. Nkamia amesema kuwa watu wengi na waoga wa kutoa hoja zao kwa kufikiria wananchi watamfikiriaje hivyo kwa upande wake huwa hana woga wowote linapokuja suala la kusimamia hoja. 

HABARI ZAIDI

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi

Mohamedi Mchengerwa, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wanaozuia watumishi kupanda vyeo wakaliwa kooni

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita