Akiongea na East Africa Television hii leo jijini Dar es salaam Amani Ongera amesema, shughuli za kuomba hazijawahi kutatua mahitaji yake na kwamba anazungukwa na mazingira magumu ambapo ameitaka serikali kuhakikisha kuwa walemavu wanatengewa makazi maalumu yanayokidhi mahitaji yao pamoja na kutatua kero na changamoto zinazowazunguka
Aidha Kasimu Abdalah ambaye naye ni mlemavu wa macho anayeishi kwa kutegema kuomba ameitaka serikali kutoweka vigezo wakati wa kutoa msaada wa pikipiki yenye magurudumu matatu kwani kwa kufanya hivyo kunazidi kuwaondolea uwezo wa kujitegemea na kuondokana na matatizo yanayowakabili.