Wednesday , 25th May , 2016

Mbunge wa Mtwara Mjini Maftaha Nachuma CUF ameliambia bunge mjini Dodoma kwamba wanafunzi wanaosoma shule za sekondari
za serikali hupewa chakula kisichofaa jambo ambalo ni hatari kwa afya yao na masomo yao kwa ujumla.

Nachuma ameyasema hayo wakati akiuliza swali la nyongeza kuhusu namna ambavyo serikali imejipanga katika kutatua kero ya chakula katika shule za sekondari.

Akijibu swali hilo naibu waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo amesema kwamba serikali ipo makini katika kusimamia jambo hilo na itahakikisha inafanya jitijhada za kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula kinachositahili kwa kujenga afya zao ili waweze kufanya vizuri kimasomo.

Aidha serikali imesema kwamba inaboresha shule ya sekondari Mchinga mkoani Lindi ili iweze kuanza kupokea kidato cha tano na sita ambapo kwa sasa serikali inatafuta fedha za kujenga mabweni na kuimarisha miondombinu ya madarasa.