
Naibu Mkurugenzi Mafunzo, Utafiti na Ushauri wa Kitaalama Chuo cha Diplomasia nchini Dkt. Kitojo Watengere amewataka viongozi kuacha mazoea ya ufanyaji kazi ambao unategemea maagizo ya viongozi wa juu na wajitume kubadilisha mfumo wa zamani ambao ukiendelea kutumika unaweza kusababishia taifa hasara kubwa ambayo itawakosesha watanzania kupata haki zao za msingi.
Dkt. Kitojo ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam, wakati akiongea na East Africa Radio, na kuongeza kuwa sambamba na mabadiliko yanayofanywa na Rais Dkt John Pombe Magufuli watanzania nao kwa nafasi zao washiriki katika kuleta mabadiliko nchini na watanzania waache malumbano ambayo hayana faida kwa nchi.