Mkurugenzi wa Umoja Switch Bw. Danford Mbilinyi.
Hatua hiyo imetajwa kuwa itasaidia kuondoa usumbufu ambapo wafanyabiashara wamekuwa wakilazimika kubeba rundo la fedha na kufuata taratibu ndefu za kibenki punde wanapohitaji pesa kwa ajili ya kulipia huduma mbali mbali au kusafiri wanapokwenda kuchukua bidhaa.
Matumizi ya mifumo hiyo yamepata baraka za Benki Kuu ya Tanzania na ile ya China na kuhusisha mfumo unaoongoza duniani wa Union Pay unaosimamiwa na serikali ya China wakati hapa nchini watumiaji wa kadi za Union Pay wanaweza kuchukua pesa kutoka benki zaidi ya 24 zilizounganishwa kwenye mtandao wa mashine zinazotumia kadi ya Umoja.
Akizungumzia kuunganishwa kwa mifumo hiyo, Balozi wa China hapa nchini Bw. Luo Youqing ame sema hiyo ni hatua muhimu itakayosaidia ukuaji wa biashara kati ya China na Tanzania, hasa ikizingatiwa kuwa Union Pay ina wateja zaidi ya milioni hamsini nje ya China, wengi wakiwa katika nchi za Ulaya na Amerika.