
Makamu wa rais Yusuph Thabit Mbalambula amesema baada ya kufanya kikao chao kwenye shirikisho lao wameamua mashindano hayo yafanyike Zanzibar mwakani baada ya mwaka huu kufanyika Bunjumbura Burundi hivi karibuni ambapo wenyeji Burundi walishinda nafasi ya kwanza na Zanzibar ikashinda nafasi ya pili.
“Baada ya kukutana shirikisho letu, tumeamua mwakani Zanzibar awe mwenyeji wa mashindano, ambapo yafanyike kabla ya mwezi wa tatu mwakani”. Alisema Mbalambula.
Katika mashindano 10 yaliopita Zanzibar imeshawahi kuwa mwenyeji katika mashindano hayo ambapo iliwahi kuandaa mwaka 2008 na mwaka 2013, mwakani itakuwa ni mwaka wa tatu kwa Zanzibar kuwa mwenyeji wa mashindano hayo makubwa ya Judo Afrika Mashariki na Kati.