
Akizungumza na www.eatv.tv muda mfupi baada ya msanii huyo kutoka BASATA, Mh. Ngereza amesema kwamba wao walichokuwa wakisisitiza kwa msanii huyo ni kuitikia wito wa Mh Shonza na siyo kumpatia hukumu.
Kwa upande wa Msanii Gigy Money amedai kwamba hakuna uhuru tena na atajitahidi kwenda kuonana na Naibu Waziri kama jinsi ambavyo BASATA walivyopmtaka kufanya.
"There is No freedom....Hakuna uhuru tena....Hakuna. Nitaongea na Naibu Waziri kama wanavyodai. Mtu anakuja kukujaji picha ya 'March' last Year...wananiambia pia hata kipindi nikiwa video vixen nilikuwa natakiwa kujitambulisha Basata, sijawahi kusikia haki ya 'video vixeni' mara ngapi nimelia mitandaoni kwa kulipwa elfu 20. Nitaongea naye naamini haki yangu itapatikana". Gigy Money
Gigy Money ni moja ya wasanii ambao waliitwa jana na Naibu Waziri Juliana Shoonza kufika ofisini kwake kwa kukiuka maadili kwenye kazi zake za sanaa.