Monday , 22nd Jan , 2018

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki Bob Junior, amekata taarifa za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii Amber Lulu akiwa mwanafunzi wa kidato cha pili.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv, Bob Junior amesema hakumbuki kuwahi kuwa na mahuisano na msanii huyo, hivyo tuhuma hizo hazina ukweli wowote.

“Hiyo sio kweli, kwanza sikumbuki na sijawahi kuwa na mahusiano na Amber Lulu, tena mwambie sitaki na sipendi kunisingizia vitu ambavyo havipo”, amesema Bob Junior.

Hivi karibuni Amber Lulu amesikika akisema aliwahi kuwa na mahusiano na msanii huyo akiwa mwanafunzi wa kidato cha pili, na ndiye aliyemtumia nauli ya kutoka Mbeya kuja Dar es salaam.