Thursday , 13th Apr , 2017

Mwanamuziki Chipukizi kutoka lebo ya 'Tetemesha Entertainment'  anayetamba na  ngoma ya 'ziwafikie' Coyo amefungukia skendo ya kuiba mashairi ya Big Jahman na kudai hata wimbo wenye hayo mashairi hajawahi kuhusikia kabla ya ngoma yake kutoka.

Coyo amefunguka leo kwenye Planet Bongo na kusema kuwa Big Jahman ni kaka yake na hata siku alipomuita studio kwenda kutengeneza kazi hakupata fursa ya kusikiliza mashairi na kama ni neno alilolitumia kwenye wimbo wake ni maneno ya kawaida ambayo yanatumika kila siku mitaani.

"Unajua mimi nilisikia story hizo za kuiba mashairi, lakini niseme siyo mashahiri na wala sijaiba ila kuna mstari ambao niliutumia katika ngoma yangu ya njoo baadaye ulikuwa unasema 'Unanitoa kwenye Mood' ni msemo ambao upo kila mahali na kila mtu anaweza akausema. Hata hivyo Jahman aliniambia dogo umechukua mstari kwenye ngoma yangu na nikamwambia bro mbona hata ngoma yenyewe sijawahi kuisikia? sema yalikwisha kwa hiyo sijaiba kitu kwa Big Jahman" Alisema Coyo.

Katika hatua nyingine msanii huyo amesema wimbo wake huu mpya wa 'Ziwafikie' umempa nafasi kubwa sana katika jamii na kwamba umepokelewa kwa kishindo kitu ambacho kimemuongezea pia 'connection nyingi za kufanya kazi.