
Davido amesema kuwa, kupitia muziki amefanikiwa kuwasilisha kile ambacho anajisikia ndani yake, na anafurahi kuona mashabiki wanakipokea, kukikubali na kukifurahia, na msanii huyu amegusia pia kuwa, kazi nzuri kutoka kwake zitaendelea kufululiza.
Katika mahojiano haya, Davido pia akazungumzia suala la yeye kuwa msanii pekee mwenye mafanikio makubwa zaidi kutoka lebo la HKN Music, ambapo amesema kuwa mwaka huu utakuwa ni wa wasanii kutoka HKN kung'ara, wakianzia na B-Red ambaye hivi karibuni anatarajia kutoka na kazi mpya.