Monday , 8th Dec , 2014

Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Nirvana, Deogratius Kithama amefanikiwa kuibuka kidedea na kuzawadiwa tuzo ya Mwandishi Bora wa habari za mitindo kwa mwaka huu kutoka Swahili Fashion Week 2014.

mtangazaji maarufu wa kipindi cha Nirvana cha EATV Deogratius Kithama akiwa na tuzo ya SFW

Kuhusiana na tuzo hii, ambayo mtangazaji huyu alikabidhiwa jukwaani na mwanamitindo wa kimataifa kutoka Canada mwenye asili ya Kitanzania, Harieth Paul Kithama ameelezea furaha yake na pia kuwashukuru wadau wote ikiwepo timu nzima ya eNewz ambayo imeshiriki vizuri kumsapoti katika mchakato huo mzima mpaka mwisho.

Washindi wengine wa tuzo za Swahili Fashion Week ni pamoja na Millen Magese aliyeshinda tuzo ya Nembo Katika Mitindo kwa mawaka 2014, Tuzo ya Mwanamitindo Myenye Kutoa Misaada, na Martin Kadinda aliyeshinda tuzo ya Mbunifu Bora wa Mwaka wa Mavazi ya Kiume na Mwanamitindo nayekuja juu H&A Dress to impress kati ya wengine wengi.