
Wasanii wa Double M Plus Salehe Kupaza na Dogo Rama
Wakizungumza na Enewz kwa nyakati tofauti wasanii hao walieleza kuwa mkasa mzima ulitokana na kiongozi wa bendi hiyo Mumini Mwinjuma kuacha kuwalipa kwa muda mrefu na kuwapatia posho tu.
“Ni kawaida yake Mumuni kuwadhurumu wasanii kwasababu hata wasanii wake wa mara ya kwanza Double M Sound ilikuwa hivyo hivyo walikuwa wanaishi kwa posho mwisho wa siku mishahara hawakupatiwa”, alisema Salehe Kupaza
Akielezea sababu iliyomfanya amtwange mangumi bosi wake 'Muumi', Kupaza alisema kuwa ni hasira alipokuja kugundua kuwa hata wao watakuwa wametapeliwa kama alivyokuwa amefanya kwa wa mara ya kwanza 'Double M Sound'
