Saturday , 14th Mar , 2015

Maonesho makubwa ya mitindo na bidhaa za Harusi ya Harusi Trade Fair kwa mwaka 2015 yameweza kuupamba usiku wa jana katika siku yake ya kwanza.

Harusi Trade Fair 2015 - Fashion Show

Usiku wake ulipambwa na maonesho ya mitindo mbalimbali kutoka kwa wabunifu mahiri katika sekta hiyo.

Onesho hilo lilienda sambamba na zoezi la utoaji wa vyeti kwa wadau na wadhamini ambao wamefanikisha kufanyika kwa tukio hilo kubwa ikiwepo East Africa TV na East Africa Radio, mwaka huu ikiwa ni mara yake ya 6 kufanyika, zoezi ambalo limefanywa na mkuu wa wilaya ya Temeke, Mheshimiwa Sophia Mjema.

Vilevile muasisi wa maonesho hayo, Mustafa Hassanali akapata nafasi ya kutoa maneno ya shukrani, sambamba na kuelezea kuwa ipo fursa kubwa iliyopo ya kuweza kurasimisha na kuleta pamoja soko la bidhaa za harusi hapa nchini, kupitia Harusi Trade Fair.