
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Manara amesema kwa mwaka 2018, Mwanamuziki Mwanafalsa pamoja na Maua Sama wameisuuza nafsi yake vilivyo kupitia wimbo wa 'Silewi' ambao kwake ameuita ni wimbo bora wa Hip hop.
Manara ameeleza kuwa msanii wake bora wa kike ni mwanadada Nandy 'The African Princess' huku akidai kwamba wimbo wake bora wa Bongofleva anaogopa kufungiwa Basata "nikiitaja tu nnao"
Manara ameongeza kwamba mrembo wake bora kwa mwaka wa saba mfululizo ni Jokate Mwegelo ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe huku Flaviana Matata akiwa mwanamitindo bora.
Kwa upande wa filamu Manara amemtaja Jacob Stephen 'JB' kama muigizaji bora wa filamu wakiume huku Riyama Ally akichukua nafasi kwa waigizaji wakike.