Saturday , 24th Jan , 2015

Msanii wa muziki Maro wa nchini Uganda, hatimaye amefanikiwa kuhitimu masomo yake ya Shahada katika Chuo Kikuu cha Makerere,

Maro

Maro amefanikiwa kupata elimu hiyo baada ya misukosuko kadhaa katika safari yake hiyo ya kielimu na kuonesha mfano kwa jamii kuwa kila kitu kinawezekana endapo utajituma kukifanya.

Hatua hii ya Maro imegusa wengi kutokana star huyu kugundua umuhimu wa elimu baada ya kuachana nayo, na kutengana na familia na kujaribu kuingia mtaani kutafuta njia nyingine za kujiendeshea maisha mwenyewe kwa kipindi cha zaidi ya miezi 11.

Maro ambaye ni Ronals Magada kwa jina lake halisi, amekuwa moja kati ya vijana wengi ambao alifikia hatua ya kugombana na familia kwa kitendo cha kuamua kuweka shule pembeni na kuugeukia muziki ambao aliamini ndio njia pekee ya mafanikio katika maisha yake.