
Kushoto ni Marehemu Patrick na kulia ni Muna Love
Muna amesema mwanawe Patrick alikuwa mtu mwenye upendo sana kwa watoto wenzake lakini pia amesema Patrick alikuwa mtu wa dini ambaye alimsababisha yeye kuokoka hivyo ameona sio mbaya akasaidia watoto wasio na uwezo na wenye maradhi mbalimbali.
"Naiomba Serikali isaidie kutoa bima ya afya kwa watoto hata kama wakiwa wanaumwa mahosipitalini ili kuweza kurahisisha matibabu kwa watoto kwa kuwa nimekutana na changamoto kubwa ya kuchelewa kwa kadi za bima ya afya katika kuzifuatilia mpaka zitoke pale unapomkatia mtoto ambaye tayari ni mgonjwa, lakini pia naomba serikali ipunguze siku za kusubiri hiyo kadi ya bima kutoka siku 21 hadi siku 2 ili kuwahi matibabu" aliongea Muna Love.
Muna Love alimalizia kwa kusema kwamba kwa sasa taasisi hiyo inajishughulisha na watoto waliopo vijijini ambao wanakuwa na matatizo mbalimbali na kukimbiwa na baba zao halafu hapo baadae anawaza kufungua kituo ambacho kitakuwa kinawasaidia watoto hao.