Thursday , 17th Sep , 2015

Mtayarishaji na msanii wa muziki Nah Reel, amejitabiria nafasi kubwa zaidi katika muziki siku za mbeleni kutokana na uamuzi wake wa kuweka kila kitu pembeni ikiwepo fani yake rasmi ya Sayansi ya Kompyuta ili kudili na muziki tu.

Mtayarishaji na msanii wa muziki Nah Reel

Nahreel ameeleza kuwa, kitu cha pekee ambacho kinamuweka pembeni na muziki ni kufuatilia michezo na kucheza kidogo mpira wa kikapu - Basketball, nguvu na akili nyingi zaidi za mkali huyo zikiwa ni katika kusuka biti kali na kufanya muziki vilevile.