Sunday , 30th Dec , 2018

Kwa mara ya kwanza tangu atoke gerezani kwa dhamana, Video Queen, Mascat Abubakary 'Amber Rutty' ameibuka na kueleza kuwa jela hapana mchezomchezo, na watu wasitamani.

Video Queen, Mascat Abubakary 'Amber Rutty'.

Amber Rutty amesema maisha ya jela siyo mazuri ndiyo maana tangu atoke kwa dhamana amekuwa na matatizo ya kiafya na kisaikolojia, na kwa sasa hajawa sawa kwaajili ya kuelezea kiundani kuhusu alichojifunza huko jela kwani hali yake bado haijatengamaa na kwamba akirudi katika hali yake ya kawaida ataeleza mengi lakini kifupi watu watambue kuwa jela siyo mahali pazuri hivyo wawe makini.

Kiukweli tangu nimetoka jela nimekuwa nikiumwa sana, yaani afya yangu siyo nzuri,  na ukweli kuwa afya yangu siyo nzuri pia kisaikolojia siko sawa, hivyo nikiwa vizuri ndiyo nitaongea mengi", amesema Amber Rutty.

Amber Rutty na mpenzi wake wanakabiliwa na mashtaka matatu yakiwemo ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile na kusambaza picha za ngono kupitia mitandao ya kijamii ambapo kesi yao bado inaendelea kuunguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu sasa wako nje kwa dhamana.

Kabla ya dhamana hiyo, wawili hao walisota katika Gereza la Segerea kwa siku 25.