Tuesday , 18th Mar , 2014

Rapa Octopizzo wa nchini Kenya, ameendelea kushuhudia mafanikio katika muziki wake siku hadi siku, ambapo msanii huyu hivi karibuni ataelekea huko Berlin nchini Ujerumani kwa ajili ya ziara ya wiki mbili ya kimuziki.

Msanii huyu atatumia ziara hii kutangaza zaidi kazi zake, ambapo kupitia ujumbe wake katika ukurasa wake wa facebook, ametangaza pia ujio wake mpya wa kazi inayokwenda kwa jina “I Do It” itakayotoka hivi karibuni.

Octopizzo amesema kuwa, ziara hii pia ni ushahidi mwingine ambao unamuaminisha kuwa kushindwa kwake na kupatwa na msongo katika kipindi cha nyuma, ilikuwa ni hatua ya msingi ya kumjenga kufikia maisha poa ambayo anaishi na kuyafurahia sasa, huku akitaka mashabiki wake kufahamu kuwa inawezekana kufanikiwa.