Thursday , 27th Feb , 2014

P Square, wameendelea kuwa mfano katika kuonyesha wanamuziki njia nyingine za kuongeza kipato chao, na hii ni kufuatia hatua yao mpya na ya kiubunifu ya kutengeneza kipindi cha televisheni cha muendelezo ambacho kipo katika muundo wa katuni, chenye visa kuhusu maisha yao.

Mastaa hawa wamekipatia kipindi hiki jina The Alingos na wamekuwa wakikitayarisha kwa miezi kadhaa sasa, na kwa mujibu wa taarifa za awali mzigo mzima umekamilika na utaanza kuruka hewani hivi karibuni kwa ajili ya burudani zaidi kwa mashabiki wao.

Mzigo huu mpya kutoka kwa P Square, umelenga zaidi kuwafikia watoto na kuwajengea moyo wa mafanikio wasanii wachanga kwa kuwaonyesha hali halisi katika mchakato mzima wa harakati za muziki Nigeria, Afrika na Duniani kwa ujumla.