
Lamar amefunguka juu ya kile anachohisi kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kuwa yeye hakuwa na nia mbaya isipokuwa ni kuonesha ni jinsi gani anakubali kazi za producer huyo, lakini yeye ameelewa vibaya na kufikiri anatumia kazi zake kutengeneza muziki.
" Kwanza Scott Storch ni producer ambaye namfuatilia toka 1999, amekuwa ameniispire nilipokuwa naanza production, nilikuwa nasikiliza beat yake nikawa napata idea, ikawa kama icon for me, na yeye sasa hivi anafanya come back kwa hiyo nikawa insipired na ile beat nikaona niirudie yani niipige niongezee vitu, alafu nikamtag"
Ameendelea kusema "Mi sijachukua beat yake, mi nimetumia beat yake alafu nikamtag yeye ingekuwa sijamtag sawa, lakini nimeonesha nimekuwa insipired na yeye, labda ingekuwa nimeitumia nimeiuza nimempa msanii, lakini nimemtag nikasema kwamba he is an isipiration alafu nikamjibu keep on insipiring us, lakini jamaa hajaelew", alisema Lamar.
Pamoja na hayo watu wengi nao wameoneshwa kutofurahishwa na kitendo cha producer huyo wa Marekani, kwa kudhania Lamar amechukua beat yake na kuitumia, na kutoa yale ambayo wanaita ya moyoni.
hajjarpamba_007: Huyu jamaa kwa sasa hayupo kwenye position nzuri amepoteza 70million dollars. Kwa hiyo sikuizi amekua serious kinoma @lamarfishcrab
nurahtumaini: I cant stay silent on this@ scottstorchoffial is wrong,let u know your the super music producer in the world so u inspire most of the young generation in music industry,so u have to feel blessed brother.wellcome in Tz.@lamarfishcrab hiyo beat wape B.O.B.