
Muigizaji Riyama Ally
Riyama amebainisha hayo baada ya watu kumuona katika video ya muziki ya msanii wa bongo fleva Leo Mysterio ambaye ndiyo mume wake huku wakidai kuwa wivu wa Riyama ndiyo umempelekea mpaka kuwa video quen katika nyimbo hiyo.
"Aliyeshauri ni mwenyewe Mr. Leo Mysterio, alisema mimi ndiyo nataka wewe uwe 'video quen' nikamwambia hapana, mbona wapo wasichana wazuri wengi tuwachukue wanaojulikana na wasiojulikana na wapo kwa ajili ya kazi hii akasema hapana huu wimbo una stori na unakuhusu wewe, basi na mimi nikaangalia nikaona video kweli inani hitaji", alisema Riyama.
Pamoja na hayo, Riyama amesema hawezi kuwaogopa video 'queen' kwa kuwa wao ni wanawake na yeye ni mwanamke.
Mtazame hapa chini akifunguka zaidi