
Msanii Godzilla
Zilla amesema hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuulizwa chanzo cha ugomvi wake yeye na msanii Nikki Mbishi pamoja na Wakazi kwa kudai kwamba hawajagombana kama watu wanavyodhania ila tatizo ni kwamba hamuelewi namna alivyo.
"Nikki 'is my friend' tumefanya kazi kwenye nyimbo yake, 'i don't know' sijui kitu gani kimetokea lakini 'we still friend. Mimi sina tatizo kwa sababu kama ingekuwa chochote kimetokea watu tusingefanya kazi pamoja, lakini imekuwa 'too much'.. Unajua watoto wa Ukonga wengi wanakuwa miyeyusho miyeyusho lakini ni ndugu zangu wakina Wakazi, Nikki tunawalea tutafanyaje wanetu hao" alisema Godzilla kupitia eNewz ya EATV.
Mtazame hapa Godzilla anavyofunguka zaidi;