
Mjadala huo umeanzishwa na raia wa Zimbabwe, Shelton Mpala,ambaye amewataka Waafrika kusaini na kupinga kitendo cha kampuni ya Disney kutumia msemo huo kama alama yao ya kibiashara kwenye filamu ya The Lion King, ambayo wanatarajia kuitoa tena mwaka 2019 ikiwa imeboreshwa.
Mzimbawe huyo amesema kitendo cha Walt Disney kutumia 'Hakuna Matata' kama alama yao ya kibiashara, ni ukoloni na unyonyaji, kitendo ambacho kimeonekana kuungwa mkono na Waafika wengi kwenye mitandao ya kijamii, huku saini ya mtandaoni 'petition' aliyoianzisha kupata zaidi ya sahihi 36,000 za kuunga mkono suala hilo.
Hey everyone, pls RT this petition for @DisneyStudios to be barred from trademarking #HakunaMatata. It's a Swahili phrase that we've used since time immemorial but white people still be trying to steal even after our independence. #Shame! pic.twitter.com/kSrUm360BV
— Mwikali Mutune (@Mwikali_Mutune) December 10, 2018
Kenyans! Wake Up! First was “Kikoi”, now “Hakuna Matata”, STOP this intellectual robbery of our culture and heritage! Sign a petition to protest @Disney’s trademarking of the kiSwahili phrase #HakunaMatata https://t.co/mm8FrIs7wg
— mapinduzi (@MaasaiNation) December 17, 2018
#HakunaMatata belongs to Africa - it belongs to the Swahili speakers in Africa
Disney trying to trademark this well-known Swahili phrase
Please Sign The Petition to stop this nonsense! https://t.co/8bEltEsVkJ—Reimagine SA (@Gaiafrique) December 19, 2018
Walt Disney ambayo hutengeneza filamu za watoto, hutumia msemo wa 'Hakuna Matata' ambao asili yake ni nchi za Afrika Mashariki, kama nembo ya kibiashara ya filamu hiyo, ambayo pia inaelezea maisha ya familia ya Kifalme ya Simba anayepatikana barani Afrika, huku majina mengi ya wahusika wakitumia yenye asili ya Afrika.
Mpaka sasa kampuni hiyo haijajibu tuhuma hizo, iwapo itakubalki kuacha kuutumia ama la.