Tuesday , 11th Mar , 2014

Waandishi wakubwa na wakongwe wa mashahiri kutoka Nigeria, akiwepo Profesa Wole Soyinka, Uzor Maxim Uzoatu, Obari Gomba na Ikeogu Oke, wamechaguliwa kutumia kazi zao kwa ajili ya kuchapishwa katika kazi kubwa kabisa ya ushahiri duniani.

Kazi hiyo kubwa ya ushairi duniani ambayo itawakutanisha wakongwe hao imepatiwa jina The Second Genesis: An Anthology of Contemporary World Poetry.

Mbali na kazi ambazo zitawasilishwa na washahiri wenzake, Professa Soyinka ambaye ana rekodi ya kupata tuzo ya amani ya Nobel, atawasilisha kazi yake ya ushahiri yenye jina "A Vision of Peace" kwa ajili ya kuhamasisha amani duniani.

Mratibu wa mpango huu atakuwa ni Dr. Moizur Rehman Khan ambaye ametajwa kuzingatia viwango vya kazi za washahiri hawa pamoja na uwezo wa miaka mingi ambao wamekuwa wakuonyesha katika fani hii.