Thursday , 6th Apr , 2017

Msanii wa Hip Hop Wakazi anayetamba na ngoma tofauti kama 'Sitaki shari pamoja na Sijutii' aliyomshirikisha Rubby amewataka wasanii wenzake kuheshimiana kimuziki na kwamba kila mmoja anautashi wake aliojaaliwa kwenye fani hiyo.

Wakazi

Siku chache zilizopita Wakazi alinukuliwa akisema hayo baada ya maneno ya 'diss' yaliyowahi kurushwa na msanii Nash MC kwenda kwa Profesa Jay na kudai kuwa katika misimamo ya maisha yake anaamini hakuna mtu anayekosea wala mkamilifu bali kinachotakiwa kwenye sanaa ni heshima kwa wote ili kukuza muziki.

Wakazi amesema tatizo la utunzi lipo na kwamba wengi wao wamekariri hip hop ni kutoa elimu pekee, huku akiongeza kuwa muziki huo ni mpana ambao licha ya kutoa elimu bado unatakiwa kuburudisha na wakati huo huo ni biashara hivyo watu hawapaswi kuwadharau wanafanya hip hop biashara na wale wanaofanya burudani.

"Tatizo lipo kwenye mitazamo lakini mtazamo wa msanii lazima uangalie unawaelimisha watu, unaburudisha na pesa unaingiza mfukoni tatizo linakuja pale mtu anapoangalia upande mmoja na kumuona mwenzake amekosea siyo poa. Ubora wa msanii ni pale unapoweza kufanya vyote kwa pamoja mfano mimi ukinipa hata beat ya mdundiko lazima nikalishe mashairi kwa sababu nina uwezo huo. Hivyo ni lazima sisi tuwaheshimu wakongwe na wakongwe watuheshimu sisi". Alisema Wakazi

Pamoja na hayo Wakazi amedai kama msanin ameweza kuzunguka mazingira tofauti tofauti kwenye jamii lazima atajua njia za kufanya muziki huo lakini kama mazingira ni yale yale lazima itokee msanii kujiona yeye ni bora kuliko mwingine.

Aidha msanii huyo amefunguka na kudai suala la msanii gani mkali waachiwe mashabiki na kuongeza kwamba historia ichwe itajieleza.