Friday , 8th Jan , 2016

Wasanii Mandojo pamoja na Domokaya wameamua kuanza mwaka kwa mtindo tofauti ambapo mbali na uwekezaji mbalimbali waliofanya katika biashara wameamua kufungua studio ya muziki kwa lengo ya kusaidia wasanii wengine kufikia mafanikio kimuziki.

Wasanii wa muziki nchini Mandojo pamoja na Domokaya

Akiongea na eNewz kwa niaba ya Domokaya, Mandojo amesema kuwa studio yao ipo wazi kwa wasanii chipukizi wenye uwezo na kutaka kuendeleza vipaji vyao vya muziki.

Inasimama kwa jina Vaku na itakuwa inasimamiwa vizuri kwa upande wa kutayarisha muziki,
na wao binafsi pamoja na watayarishaji mbalimbali ambao watakuwa wakifika kufanya kazi pamoja.