Friday , 5th Jun , 2015

Wachezaji 21 wa mchezo wa Judo wanatarajia kuingia kambini hivi karibuni kwa ajili ya mchujo wa kutafuta timu ya taifa itakayoshiriki michuano ya All Africa Games inayotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu nchini Congo Brazzaville.

Katika taarifa yake, katibu mkuu wa Chama cha Judo nchini JATA, Innocent Malya amesema, wachezaji hao wamepatikana kutoka klabu za Tanzania bara na Zanzibar ambao wataingia kambini kwa ajili ya kupata timu ya taifa ya mchezo huo.

Malya amesema, chama cha Judo Zanzibar ZJA kimefanya uteuzi wa wachezaji watakaoiwakilisha Zanzibar na hivyo JATA wameteua wachezaji watakaoiwakilisha Tanzania Bara.

Malya ameswema, wachezajji wote wanatakiwa kuingia kambini na kufanya mazoezi ya pamoja na kila uzito atachaguliwa mchezaji mmoja mwenye kiwango cha juu cha kuunda timu ya Taifa itakayoshiriki michuano ya All Africa Games.