Tuesday , 16th Jan , 2018

Habari kubwa hivi sasa kwenye tetesi za usajili barani Ulaya ni ile inayomuhusu mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang wa Dortmund anayehusishwa kujiunga na Arsenal.

Mpango huo wa Arsenal kumsajili nyota huyo raia wa Gabon huenda ukawa unakaribia kukamilika baada ya loe Aubameyang kuonekana kwenye video akilisifia jiji la London na kuomba kupelekwa jijini humo.

Video hiyo imewekwa kwenye kipengele cha 'Story' kupitia ukurasa wa mtandao wa Instagram wa mchezaji  mwenzake wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho ambaye ni raia wa England na mwenyeji wa jiji la London.

Aubemeyang ameonekana na kusikaka kwenye video hiyo akisema ''utanipeleka London siku moja, nikafurahie tu kwasababu umeniambia London ni sehemu nzuri sana".

Arsenal inajitahidi kutaka kukamilisha usajili huo kwaajili ya kuziba nafasi ya winga Alexis Sanchez ambaye anaripotiwa kutaka kuondoka kwaajili ya kujiunga na klabu ya Manchester United.