Thursday , 29th Nov , 2018

Rapa mkongwe kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, AY a.k.a mzee wa Comercial amesema anajivunia kuwa msanii mwaminifu jambo ambalo lilimpa nafasi ya kufanya kazi na wasanii wengi wakubwa wakiwemo Psquare.

Peter Psquare, Ay na Paul Psquare

Kupitia Planetbongo ya East Africa Radio, AY amesema yeye hasimamii wasanii kama watu wengi wanavyodhani lakini anachokifanya ni kutoa mashavu kwa washkaji ikiwemo kuwaunganishia collabo pamoja na show.

''Niliwahi kuwapa mchongo Psquare walikuwa na Show Burundi lakini hawakuwa na mwenyeji kwahiyo mimi nikawaunganisha na mtu akasimamia kila kitu, kwahiyo mimi nilikuwa kama niko 'Back Stage'  na jamaa wakafanya show na wakapewa mzigo wao'', amefunguka AY.

AY ambaye alikuwa msanii wa kwanza kuufanya muziki wa Hip hop uwe na sura ya kibiashara 'Hip hop commercial' amesisitiza kuwa pamoja na ukubwa wake anaheshimu sana 'Media' na ndio maana kila akiachia ngoma lazima afanye 'Media tour'.

Mkali huyo wa kitambo kwenye 'game' ameachia ngoma yake mpya inaitwa 'Safari' akiwa amemshirikisha mkongwe mwingine wa muziki Bongo, Mzee King Kiki.