Abdul ameyasema hayo leo kwenye hafla ya kusaini mkataba wa timu hiyo kuendelea na udhamini na Benki ya NMB ambayo imekuwa ikiwadhamini kwa misimu mitatu mfululizo.
'Udhamini huu unatuongezea nguvu kwenye mapambano yetu katika michuano ya ligi kuu na huu mwaka unaonekana kuwa ni wa kwetu hivyo tutaendelea kufanya vizuri na mwezi wa tano tunaweza kuibuka mabingwa'', amesema Abdul.
Azam FC sasa itaendelea kudhaminiwa na NMB kama mdhamini mkuu kwa mwaka mwingine wa nne baada ya leo kusaini makubaliano hayo kwenye mkutano uliofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam leo.
Mabingwa hao wa kombe la Mapinduzi, wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 30. Vinara wa ligi ni Simba SC ambao wana alama 32 wote wakiwa wamecheza mechi 14.







