Monday , 18th Jul , 2016

Kocha mpya wa Azam FC, Mspaniola Zeben Hernandez Rodriguez ameanza kwa ushindi wa mabao 2-0 asubuhi ya leo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Ashanti United ya Daraja la Kwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Kiungo Mudathir Yahya alianza kuipatia timu yake bao la kwanza katika dakika ya 69 kwa shuti la kiufundi kufuatia pasi ya kiungo Frank Domayo.

Abdallah Masoud 'Cabaye' akawafungia bao la pili dakika ya 81 mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa shuti zuri la umbali wa mita 30.

Kocha Rodriguez alipanga vikosi viwili tofauti kipindi cha kwanza akiwaanzisha Juan Jesus Gonzalez, Wazir Salum, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Himid Mao, Kipre Bolou, Jean Mugiraneza, Ramadhani Singano 'Messi', Ibrahima Fofana, Shaaban Idd na Salum Abubakar 'Sure Boy' ambao wote aliwatoa kipindi cha pili na kuingiza wengine.

Kikosi cha Azam kilikuwa; Juan Jesus Gonzalez/Aishi Manula dk 46, Wazir Salum/Gadiel Michael dk 46, Erasto Nyoni/Abdallah Kheri dk 46, Aggrey Morris/Ismail Gambo dk 46, David Mwantika/Himid Mao dk 46, Michael Bolou/Frank Domayo dk 46, Jean Mugiraneza/Mudathir Yahya dk 46/Himid Mao dk 77, Salum Abubakar/ Abdallah Masoud ‘Cabaye’ dk 46, Ramadhan Singano/Khamis Mcha dk 46, Ibrahima Fofana/Kelvin Friday dk 46, Shaaban Idd/AmeAlly dk 46 .