Saturday , 26th Jan , 2019

Mlinda mlango wa Yanga Beno Kakolanywa, ambaye amewekwa kando na kocha wa kikosi hicho Mwinyi Zahera, ametakiwa kwenda kumuomba msamaha kocha huyo ili aweze kumsamehe na kumpa nafasi tena.

Beno Kakolanya

Beno amepewa ushauri huo na mchezaji wa zamani wa Yanga Stephano Mwasyika ambaye amemtaka kumaliza tatizo lake na kocha kwa kuomba msamaha.

''Mdogo wangu muombe mwalimu msamaha maisha yaendelee'', ameandika Mwasyika ambaye amewahi kuichezea Ruvu Shooting.

Mwishoni mwa mwaka 2018, Zahera alifukuza Beno kikosini na kumtaka atafute timu nyingine kutokana na mlinda mlango huyo kushinda kurejea kikosini baada ya kutoka kwenye kambi ya timu ya taifa akishinikiza kulipwa fedha zake anazoidai klabu.